Home kimataifa POCHETTINO ATAJA SABABU ZA KUMTOA MESSI

POCHETTINO ATAJA SABABU ZA KUMTOA MESSI


 MAURICIO Pochettino, Kocha Mkuu wa Paris Saint Germain, (PSG) amesema kuwa sababu kubwa ya kumtoa Lionel Messi kwenye mchezo wao dhidi ya Lyon ilikuwa ni kumlinda dhidi ya majeruhi.

Messi alikwama kuyeyusha dakika 90 kwenye mchezo huo wa Ligue 1 uliochezwa Uwanja wa Parc des Princes, dakika 90 ulisoma PSG 2-1 Lyon. Ilikuwa ni mabao ya Neymar Jr dakika ya 66 kwa mkwaju wa penalti na Mauro Icard dakika ya 90 alifunga bao la ushindi na kwa wapinzani wao Lyon bao lilipachikwa na Lucas Paqueta dakika ya 54.

Messi alipotolewa dakika ya 73 alionyesha bonge moja ya mnuno kwa kuwa hakuwa na furaha kutolewa kwenye mchezo na mpaka sasa baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya Barcelona akiwa amecheza mechi nne hajacheka na nyavu.

Pochettino amesema kuwa aliamua kufanya maamuzi magumu kwa kuwa kuna mechi ngumu mbele zinakuja ikiwa ni pamoja na zile za kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo lilimfanya aweze kumtoa Messi.Kesho PSG inatarajiwa kucheza na Klabu ya Metz kwenye mchezo wa ligi.

“Kuna maamuzi unatakiwa kufanya kwa ajili ya timu na nilifanya hivyo kumtoa Messi kwa sababu ya kumlinda na kuhofia majeruhi. Tuna mechi muhimu mbele ni lazima nimlinde,” amesema.

SOMA NA HII  BENZEMA AFIKISHA MABAO 71 UEFA, ZIDANE MATUMAINI KIBAO