Home news SIMBA WAREJEA DAR USIKU WAKITOKEA ARUSHA

SIMBA WAREJEA DAR USIKU WAKITOKEA ARUSHA


KIKOSI cha Simba kimewasili Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Septemba 18 kikitokea Arusha ambapo kilikuwa huko kwa kambi ya pili.

Kambi ya kwanza ilikuwa Morocco na ilipomeguka waliweka kambi ya pili Arusha ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.

Kwa sasa kimerejea ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya kukamilisha tamasha lao la Simba Day ambalo linatarajiwa kufanyika kesho, Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Klabu ya TP Mazembe ambao ni mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Pia itakuwa ni siku ya tambulisho rasmi wa jezi mpya ya Simba itakayotumika kwa msimu wa 2021/22 pamoja na wale Mascot ambao wanaitwa Mo RAFIKI.

Kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ameweka wazi kuwa hakutakuwa na mchezo mwingine mpaka pale watakapocheza mchezo wao dhidi ya TP Mazembe.


SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...AZAM WATAKA KUFANANA NA SIMBA KILA KITU...NAO WAPANGA KUIFUATA AL AHLY...