Home news UNAAMBIWA ILIBAKI KIDUCHU TU..SAMATTA ACHEZE ‘SAKO KWA BAKO’ NA MESSI..MCHONGO ULIKUWA HIVI

UNAAMBIWA ILIBAKI KIDUCHU TU..SAMATTA ACHEZE ‘SAKO KWA BAKO’ NA MESSI..MCHONGO ULIKUWA HIVI


ILIBAKI kidogo tu msimu huu kumshuhudia nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akicheza Ligi moja na mshindi mara sita wa tuzo za Ballon d’Or, Lionel Messi.

Kabla ya kufanya maamuzi ya kurejea Ubelgiji, Samatta alikuwa kwenye rada za klabu mbili zinazoshiriki Ligi Kuu Ufaransa ambazo ni Troyes na Montpellier.

Klabu hizo zilionyesha nia ya kutaka kumsajili Samatta na kwa mujibu wa ripoti kutoka Ufaransa, zinaeleza kwamba Montpellier waliweka mezani kitita cha Euro 2.5milioni ambazo ni zaidi ya Sh. 6.8 Bilioni ili kumnasa mshambuliaji huyo.

Walichofanya Royal Antwerp ni kuweka mzigo wa maana ambao ni Euro 4milioni ambazo ni zaidi ya Sh. 10.9 bilioni, mzigo huo ulionekana kuwavutia Fenerbahce na kuamua kumruhusu nahodha huyo wa Taifa Stars kurejea zake Ubelgiji ambako alijipatia umaarufu mkubwa kabla ya kwenda England ambako mambo hayakuwa mazuri.

Kama Troyes na Montpellier wangeamua kuendelea kumkomalia huenda tungemshuhudia pengine Samatta akicheza Ligi moja na Messi ambaye amejiunga na PSG akitoka FC Barcelona ya Hispania lakini jambo hilo liliota mbawa siku ya mwisho ya usajili.

Samatta , anakuwa mchezaji wa saba kutoka Afrika katika kikosi cha Brian Priske. Wengine ni pamoja na Abdoulaye Seck (Senegal), Alhassan Yusuf (Nigeria), Nill De Pauw na Luete Ava Dongo (DR Congo), Bruny Nsimba (Angola) na Opoku Ampomah (Ghana).

SOMA NA HII  ALIYELETA JEZI FEKI SIMBA, YANGA KUANIKWA HADHARANI LEO