Home news VIJANA WA SIMBA WALIOIPA TABU AL AHLY WASEPA JUMLAJUMLA

VIJANA WA SIMBA WALIOIPA TABU AL AHLY WASEPA JUMLAJUMLA


PITSO Mosimane,  Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sasa msimu wa 2021/22 atakuwa na kijana wake anayekubali uwezo wake ambaye ni Luis Miquissone. 


Pia nyota wawili ambao waliipa tabu Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa walipokutana wamesepa jumlajumla ndani ya kikosi cha Simba.

Ni Luis ambaye alikuwa anaitumikia Simba msimu wa 2020/21 na alikuwa miongoni mwa wale walioipa tabu timu hiyo yenye mkwanja wa kutosha Afrika.

Wakati ubao ukisoma Simba 1-0 Al Ahly ni Luis aliachia shuti kali kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwa shangwe kubwa jukwaani.

Mwingine ambaye naye amesepa na kuibuka ndani ya RS Berkane ya Morocco ni mtoa pasi ya mwisho kwa Luis anaitwa Clatous Chama wengi wanapenda kumuita Mwamba wa Lusaka.

Ilikuwa ni Februari 21 katika mchezo wa hatua ya makundi ambao ulikuwa na ushindani mkubwa huku Simba walikuwa wakipewa nafasi kiduchu ya kushinda mchezo huo.

Licha ya Simba kushinda mchezo huo waliweza kuwazidi mabingwa hao mara 10 wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika suala zima la umiliki wa mpira pamoja na pasi za kutosha.

Rekodi zinaonyesha kuwa Simba walipiga jumla ya pasi 451 na Al Ahly walipiga pasi 425 na kwa upande wa umiliki wa mpira Simba ilikuwa ni asilimia 51 na Al Ahly ilikuwa ni asilimia 49.


SOMA NA HII  MKWANJA WAKO UPO KWENYE LIGI KUU INDIA, TAZAMA ODDS ZA USHINDI!