Home news YANGA YAPIGA HESABU YA KUTWAA MAKOMBE

YANGA YAPIGA HESABU YA KUTWAA MAKOMBE


HERITIER Makambo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa malengo makubwa kwa msimu wa 2021/22 ni kuweza kusepa na mataji ambayo watashiriki ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara.

Makambo amerejea ndani ya Yanga aliyokuwa akiitumikia msimu wa 2018/19 kabla ya kuibukia ndani ya Horoya ya Guinea.

Waliweza kufikia makubaliano ya kuachana pande zote mbili kwa kuwa dili lake lilikuwa limebakiza mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo.

Baada ya kureja ndani ya Yanga inaelezwa kuwa ni dili la miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia. 

Makambo amesema:”Tupo imara na kwa namna ambavyo timu ipo tuna uhakika tutafanya vizuri, tunahitaji kuchukua makombe kwenye mashindano ambayo tutashiriki.

“Ipo wazi kwamba haitakuwa rahisi lakini ni lazima tujitume zaidi na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” .

Wakati anasepa nyota huyo alikuwa ni namba moja kwa utupiaji ambapo alitupia mabao 17.Anareja na kukuta namba moja kwa utupiaji kwa msimu wa 2020/21 ni Yacouba Songne ambaye alitupia mabao 8.

Mabingwa wa msimu uliopita wa 2020/21 ni Simba ambao pia walitwaa taji hilo zama zile wakati akisepa na timu ilimaliza ikiwa nafasi ya pili kama ambavyo ilifanya hivyo pia msimu uliopita.


SOMA NA HII  AUSSEMS AZIVURUGA KLABU ZA KENYA NA RWANDA....ADAIWA KUSAINI MKATABA BILA KUAGA...