Home news YANGA YAZINDUA TAWI JIPYA KAGERA

YANGA YAZINDUA TAWI JIPYA KAGERA


 
UONGOZI wa Yanga umeweza kuzindua tawi jipya huko Kagera ikiwa ni katika hafla fupi iliyofanyika jana, Septemba 28,

Ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha ambaye aliongoza na Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara pamoja na mkuu wa msafara, Salim Rupia.

Tawi hilo jipya linaitwa Missenyi lipo wilaya ya Missenyi Mkoa wa Kagera.

Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo kina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Kagera Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, Uwanja wa Kaiataba.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa tawi hilo.

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA 'KUKIWASHA' NA WASAUZI......MZAMIRU AIBUKA NA HILI JIPYA...