KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kimataifa ambapi Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Leo wamefanya mazoezi Uwanja wa Boko na waliwasili namna hii wakiwa na mastaa wao pamoja na wale wachezaji wa timu ya U 20. Chris Mugalu, John Bocco, Bernard Morrison na Ibrahim Ajibu ni miongoni mwa mastaa ambao walikuwa katika orodha ya wale ambao wameanza mazoezi leo.