MKURUGENZI wa masuala ya michezo ndani ya Klabu ya PSG, Leonardo Araujo amesema kuwa Klabu ya Real Madrid inapaswa kupewa adhabu kubwa.
Imekuwa ikielezwa kuwa Madrid wanahitaji saini ya mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe ambaye bado ni mali ya timu ya PSG inayoshiriki Ligue 1 hivyo kitendo cha kuripotiwa kwamba amefanya mazungumzo na timu inayohitaji saini yake ni kinyume na utaratibu kwa kuwa bado ana mkataba na timu yake ya sasa.
Kiongozi huyo amesema kuwa Madrid walionyesha kutokuwa na nidhamu kwa PSG pamoja na soka kiujumla kutokana ana kuzungumza kuhusu mchezaji wa timu nyingine.
Mbappe mwenyewe aliwahi kusema kuwa anataka kuondoka PSG ili akapate changamoto mpya na timu ambayo anatajwa kwenda ni Madrid ambao wanatajwa kuwa wamekuwa wakimshawishi afanye hivyo jambo ambalo limewakasirisha mabosi wa PSG.
Taarifa imesema kuwa Madrid wapo tayari kutoa kitita cha Euro milioni 200 kwa ajili ya mchezaji huyo kinda raia wa Ufaransa.
“Nafikiri Madrid wanatakiwa kupewa adhabu kwa kuwa wamekuwa wakipambana tu kila siku kuwa wanataka kumsajili Mbappe ambaye wanafahamu kwamba ana mkataba na PSG,”.