Home news OMONG WA MTIBWA SUGAR AKWAMA KUANZA KAZI

OMONG WA MTIBWA SUGAR AKWAMA KUANZA KAZI



LICHA ya kutambulishwa rasmi kukinoa kikosi cha Mtibwa Sugar kwa msimu wa 2021/22, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog ameshindwa kuiongoza timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Bara baada ya vibali vyake vya kazi kutokuwa sawa.


Mtibwa ikiwa tayari imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikianza kwa kufungwa 1-0 na Mbeya Kwanza kabla ya kuambulia suluhu na Prisons, timu hiyo imekuwa ikiongozwa na kocha msaidizi, Awadh Juma, huku Omog akiwa jukwaani.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: “Ni kweli kocha wetu Omog hajasimamia mchezo wowote wa ligi mpaka sasa na sababu kubwa ni vibali.

“Vibali vyake vya kazi vimecheleweshwa na Serikali ila tunavifanyia kazi na tuna imani baada ya wiki hizi mbili wakati ligi imesimama vitakuwa vimepatikana na ataanza kazi rasmi.”


SOMA NA HII  MATOLA :- TUNAENDA KUTIBUA REKODI IVORY COAST....MECHI NI NGUMU MNOOO...