Home news TWIGA STARS WANA ‘MZUKA’ KAMA WOTE….WAKAMILIKA KUIMALIZA NAMIBIA KWAO

TWIGA STARS WANA ‘MZUKA’ KAMA WOTE….WAKAMILIKA KUIMALIZA NAMIBIA KWAO

 


Kikosi cha timu ya taifa ya Wanawake Twiga Stars, leo Ijumaa (Oktoba 22), kimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika dhidi ya Namibia.

Mchezo huo utachezwa kesho Jumamosi (Oktoba 23) Uwanja wa Dobsonville, Soweto Afrika Kusini.

Kuelekea mchezo huo, Twiga Stars wana deni la kulipa, kufuatia kupoteza mpambano wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Jumatano (Oktoba 20) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Twiga Stars ilikubali kufungwa mabao 2-1, hali inayoifanya kusaka ushindi wa mabao 2-0 kwenye mpambano wa kesho Jumamosi (Oktoba 23) ili kujihakikishia nafasi kusonga mbele.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Twiga Stars.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI LEO....GAMONDI ATAJA SILAHA ATAKAYOITUMIA KUIMALIZA SIMBA MAPEMA...