Home Uncategorized JOSE MOURINHO AMTAKA JIMEZEZ WA WOLVES

JOSE MOURINHO AMTAKA JIMEZEZ WA WOLVES


RAUL Jimenez, mshambuliaji wa Klabu ya Wolves yupo kwenye hesabu za Kocha Mkuu wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho anayemtaka ndani ya kikosi chake.

Nyota huyo wa Wolves raia wa Mexico mwenye miaka 29 amemvutia Mourinho ambaye anaamini kuwa atakuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi chake hasa kwa nafasi ya utupiaji mabao.

Mourinho, anaamini kuwa atakuwa na pacha matata akiungana na mshambuliaji wake Harry Kane, huku kigezo cha umri kuwa mkubwa kikitajwa kuwa kitapunguza gharama ya kumpata.

Ametupia jumla ya mabao 22 akiwa na pasi 10 za mabao akiwa amecheza jumla ya mechi 44 msimu huu Kwenye mashindano yote kiujumla.

SOMA NA HII  SIMBA NI NGUMU ILA INAFUNGIKA