Home news YANGA WAIBUKA NA MKAKATI MPYA WA KUIVUA UBINGWA SIMBA..MECHI ZA UGENINI ZATAJWA

YANGA WAIBUKA NA MKAKATI MPYA WA KUIVUA UBINGWA SIMBA..MECHI ZA UGENINI ZATAJWA


UONGOZI wa Yanga umepanga kuja na mikakati mipya itakayowapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.

Msimu huu, Yanga tayari imecheza michezo miwili ya ligi ambayo yote wamefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli, alisema kuwa moja ya mkakati waliouweka msimu huu ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo wa ugenini.

Bumbuli alisema kuwa lengo ni kupata pointi tatu katika kila mchezo, hilo linawezekana kutokana na usajili bora walioufanya msimu huu.

“Tumekuja na mpango mkakati ambao wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wanafahamu, kikubwa ni kufanikisha malengo yetu ya msimu huu.

“Hatutaki kuacha pointi yoyote tunapokuwa ugenini ambako kuna viwanja vibovu. Hatutaki kurudia makosa tuliyoyafanya msimu uliopita. tukipata pointi tatu ugenini basi na nyumbani hatutaki kuacha pointi yoyote,” alisema Bumbuli.

SOMA NA HII  ISHU YA MAKAMBO NA YANGA IMEFIKIA HAPA