Home news HITIMANA AAMUA KUWEKA UNAFIKI PEMBENI..AFUNGUKA HAYA KUHUSU UWEZO WA PABLO…

HITIMANA AAMUA KUWEKA UNAFIKI PEMBENI..AFUNGUKA HAYA KUHUSU UWEZO WA PABLO…

0


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa muda wa klabu ya Simba, Hitimana Thierry  ni kama ameamua kuweka unafiki pembeni ambapo ametoa neno kuhusu ujio wa kocha mpya wa klabu hiyo, Mhispania Pablo Franco na kusema ana imani kocha huyo ataivusha Simba kwenye kipindi kigumu kinachoipitia hivi sasa.

Hitimana amesema, โ€œNimefurahi kukutana naye naamini huu ni wakati wa kumpa muda na ushirikiano ili aweze kuitoa Simba mahala ilipo na kuipeleka mbele zaidi kama alivyofanya mtangulizi wakeโ€. 

Hitimana ameyasema hayo kocha mpya wa Simba, Pablo Franco alipowasili nchini Novemba 10, 2021 na kutembelea kambi ya wachezaji na Uongozi wa klabu hiyo maeneo ya Bunju pembeni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.