Home news AJIBU YAMKUTA SIMBA…PABLO AMUONDOA KIKOSINI MAPEMA TU…ISHU NZIMA IKO HIVI….

AJIBU YAMKUTA SIMBA…PABLO AMUONDOA KIKOSINI MAPEMA TU…ISHU NZIMA IKO HIVI….

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amemuondoa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo,Ibrahim Ajibu katika mipango yake.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa leo Ijumaa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Pablo, huo utakuwa mchezo wake wa kwanza wa mashindano kukaa kwenye benchi akiiongoza timu hiyo akisaidiana na wasaidizi wake, Thiery Hitimana na Selemani Matola.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Murtaza Mangungu ameliambia Championi Ijumaa kuwa kiungo huyo atakosekana katika mchezo huo baada ya kupata majeraha katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo.

Mangungu alisema kuwa kiungo huyo alijikwaa uwanjani akifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.

“Ajibu hatakuwepo katika sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Ruvu kesho (leo) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

“Ni baada ya kupata majeraha mazoezini, alijikwaa mguuni akiwa anakimbia na kusababisha kupata maumivu,” alisema Mangungu.

SOMA NA HII  RASMI KIRAKA WA SOKA NI MWANANCHI