Home news MCHAKATO KOCHA MPYA SIMBA WAFIKIA PATAMU…KUTANGAZWA NDANI YA SIKU 14….SIRI YAFICHULIWA…

MCHAKATO KOCHA MPYA SIMBA WAFIKIA PATAMU…KUTANGAZWA NDANI YA SIKU 14….SIRI YAFICHULIWA…


WAKATI Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kwa takribani wiki mbili, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, imepanga kutumia muda huo kushusha kocha mpya wa kuinoa timu hiyo ambayo pia inajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Novemba 28, mwaka huu, Simba itavaana na Red Arrows kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa mchezo wa kwanza wa mtoano kusaka nafasi ya kwenda makundi ya michuano hiyo, kabla ya kurudiana Desemba 5, nchini Zambia.

Jina la Kocha Mkuu wa Horoya AC ya Guinea, Lamine N’diaye, ndiyo linalotajwa kumrithi aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mfaransa, Didier Gomes.

Akizungumza na Gazeti la Spoti Xtra, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya timu hiyo, Asha Baraka, alisema kuwa bodi imepanga kumleta kocha huyo kabla ya mchezo huo wa kimataifa.

Kiongozi huyo alisema kuwa, kocha huyo huenda akakaa katika benchi kwenye mchezo huo ambao timu hiyo watahitaji ushindi.

Aliongeza kuwa wajumbe wa bodi wanatarajiwa kukutana kufanya kikao baada ya mchezo wa leo (jana) wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

“Ngumu kumleta kocha mpya bila ya maamuzi ya pamoja ya wajumbe kukubaliana kwa pamoja baada ya kupitia CV za makocha kumi waliopitishwa katika mchujo wa awali.

“Mchujo wa mwisho umepangwa kufanywa haraka mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Namungo tutakaocheza leo (jana).

“Baada ya mchujo huo kufanyika haraka kocha mpya atatangazwa sambamba na kuanza kazi katika kipindi hichi ambacho ligi imesimama,” alisema Baraka.

SOMA NA HII  IFANYE JUMAPILI YAKO KUWA YA USHINDI KWA ODDS HIZI ZA UHAKIKA NDANI YA MERIDIANBET...