Kocha wa Geita Gold Fred Felix Minziro amesema sababu ya timu yake kuishambulia sana Simba kipindi cha pili kwenye mchezo wa Ligi Kuu ni kwa sababu anajua ubora wa Simba huwa ni dakika 30 tu za mwanzo wa mchezo.
Licha ya kuonekana ni timu bora kipindi cha pili lakini Geita walipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo ambao ulichezwa katika dimba la Benjamini Mkapa Dar es salaam, mabao ya Simba yalifungwa na Peter Banda na Mzamiru Yassin na lile la Geita lilifungwa na Juma Mahadhi.
Kocha Minziro alipoulizwa kuwa alibadilisha nini kilihopelekea timu yake kuwa bora kipindi cha pili na kuwashambulia sana Simba alisema,
‘’Simba ni timu kubwa ni timu mzuri kwahiyo lazima niingie kwa tahadhali na nilijua Simba dakika zao ni dakika ya kwanza mpaka thalathini ikishapita hapo Simba inakuwa ya kawaida. Hivyo nilijaribu kupambana kwa hilo lakini ilishindikana tukaweza kutoa goli mbili, baada ya pale tukaendelea kupambano ikabidi tufunguke kama ambavyo nilifanya mechi ya Mbao nikamfunga Simba 3-2 kama mnakumbuka na leo nilifanya hivyo kipindi cha pili ikabidi nifunguke’’.
Kwa matokeo haya Simba imefikisaha alama 17 ikiwa nafasi ya pili tofauti ya alama 2 na Yanga wanoongoza Ligi wakiwa na alama 19, wakati Geita wamesalia na alama zao 5 wakiwa nafasi ya 15.