Home news KUMBE WEUPE TU….MORRISON KAMA KAWA NA VITUKO VYAKE…AZUA SINTOFAHAMU UWANJANI…

KUMBE WEUPE TU….MORRISON KAMA KAWA NA VITUKO VYAKE…AZUA SINTOFAHAMU UWANJANI…


DAKIKA 90, zilimalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wenyeji Simba kutoka suluhu ya 0-0, na Yanga.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu huku Simba ikibadilika kiuchezaji tofauti na mwanzo mwa kipindi cha kwanza cha mchezo.

Dakika ya 63, kocha wa Simba Pablo Franco alifanya mabadiliko ya kumtoa mshambuliaji Kibu Denis na nafasi yake kuchukuliwa na Larry Bwalya ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo.

Kwa upande wa Yanga Kocha Mkuu Nassredine Nabi alifanya mabadiliko dakika ya 69, ya kumtoa Jesus Moloko na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Mussa.

Dakika ya 79, Simba iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Meddie Kagere, Bernard Morrison na nafasi zao kuchukuliwa na John Bocco na Yusuph Mhilu.

Mabadiliko ya Morrison yalizua sintofahamu Uwanjani baada ya kupiga mpira wa kona bila mwamuzi kuruhusu kisha kuonyesha kutokuwa tayari kutoka wakati akijiandaa kupiga mpira wa kona uliokuwa unaelekezwa upande wa Yanga.

Dakika ya 86, Yanga iliendelea kufanya mabadiliko kwenye eneo la ushambuliaji kwa kumtoa Fiston Mayele na nafasi yake kuchukuliwa na Heritier Makambo.

Matokea hayo yanaifanya Yanga kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 20, huku ikiwa pia ni sare ya pili msimu huu baada ya kufungana bao 1-1, na Namungo FC Novemba 20.

Kwa upande wa Simba inaendelea kusalia nafasi ya pili na pointi 18, huku ikiwa sare ya pili baada ya Septemba 28, kutoka suluhu ya 0-0 na Biashara United.

SOMA NA HII  CHAMA AFUNGUKA KUHUSU HESHIMA YA SIMBA, ATAKA JAMBO HILI MSIMU HUU KWA SIMBA