Home news BAADA YA KUUONA UCHEZAJI WA USHINDI…NABI AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…ATAJA PRESHA …

BAADA YA KUUONA UCHEZAJI WA USHINDI…NABI AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…ATAJA PRESHA …


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amewapa majukumu mazito wachezaji wake akiwemo winga mpya, Chico Ushindi kwa kuwaambia wahakikishe wanapata matokeo mazuri ya ushindi katika kila mchezo uliopo mbele yao.

Yanga ambayo inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13, ndiyo timu pekee hadi sasa ndani ya ligi hiyo ambayo haijapoteza mechi.

Nafasi ya pili kwenye msimamo inakamatwa na Simba yenye pointi 24 kabla ya jana Jumamosi kucheza na Mtibwa Sugar.

Jana Jumapili, Yanga ilikuwa mgeni wa Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Shekh Amri Abeid, Arusha.

Nabi alisema bado wana safari ndefu ya kuelekea kwenye ubingwa licha ya kuendelea kupata matokeo mazuri kila kukicha, lakini amewataka wachezaji wake kuendelea kupambana kuhakikisha hawatoki nje ya mstari.

“Kitu kikubwa ambacho bado tunapaswa kukiangalia ni jinsi ya kuendelea kupata matokeo ya ushindi katika kila mchezo ambao upo mbele yetu kwa sababu ni jukumu la kila mchezaji kuhakikisha tunapata matokeo ya kufikia malengo ya ubingwa.

“Presha bado kubwa kwa sababu bado tuna mechi nyingi kwa kuwa hakuna ambaye amefikia nusu ya ligi, hivyo ni jukumu la kila mchezaji ambaye anapata nafasi ya kucheza kuhakikisha anatoa alichonacho ili kufikia malengo ya kupata matokeo mazuri kutokana na ugumu wa ligi yenyewe,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  KOCHA WA CHAMA: YANGA ITASHINDA...MASTAA SIMBA WANYIMWA POSHO..RAGE AFUNGUKA....