Home news EEHE…UMESIKIA ALICHOSEMA MUGALU HUKO SIMBA..?…AFUNGUKA A-Z YALIYOJIFICHA MOYONI…

EEHE…UMESIKIA ALICHOSEMA MUGALU HUKO SIMBA..?…AFUNGUKA A-Z YALIYOJIFICHA MOYONI…


MARA baada ya kufunga bao lake la kwanza tangu kuanza kwa msimu huu, mshambuliaji Mkongomani ndani ya kikosi cha Simba, Chris Mugalu, ameibuka na kutamka kuwa sasa hivi kasi ya mabao ndiyo imeanza, hivyo watamtambua.

Kauli hiyo aliitoa mshambuliaji huyo mara baada kufunga bao moja katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Dar City katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, juzi Jumapili.

Katika ushindi huo, mabao mengine ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere aliyefunga mawili, huku Clatous Chama, Rally Bwalya na Pascal Wawa kila mmoja akifunga moja.

Kwa mujibu wa Mugalu, bao hilo litamuongezea hali ya kujiamini baada ya kukaa muda mrefu bila ya kufunga.

“Nina furaha kubwa leo (juzi) kufunga bao langu la kwanza tangu kuanza kwa msimu huu ambao kwangu nauona mgumu tofauti na msimu uliopita.

“Lakini ninashukuru kuona nikifunga, bao hili litaniongezea hali ya kujiamini na kufunga mengi zaidi. “Kikubwa niendelee kuomba ushirikiano na umoja kutoka kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wetu kuendelea kuvumilia hiki kipindi kigumu tunachokipitia,” alisema Mugalu

SOMA NA HII  KUHUSU KUTOKUWA NA KIKOSI CHA KWANZA RASMI...MASTAA SIMBA WAFICHUA YA FADLU...