MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema mchezo wao wa leo Februari 23 dhidi ya Mtibwa Sugar wanahitaji pointi tatu na sio kitu kingine.
Mtibwa na Yanga wanacheza leo saa 10:00 katika Uwanja wa Manungu uliopo Turiani, Manungu.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi kumalizika, Manara amesema mchezo huo utakuwa mgumu lakini watatoka na pointi tatu.
Manara amesema Mtibwa wana timu nzuri na wachezaji wenye uzoefu huku kila mmoja akitaka kujitangaza.
“Kikosi cha Mtibwa kipo vizuri na wanafahamu vizuri Ligi, sisi tupo tayari kwa ajili ya mchezo na kuchukua pointi tatu,” amesema Manara na kuongeza;
“Hizi ni mbio na bado zinaendelea kwahiyo muhimu kwanza kuchukua pointi tatu.”
Yanga wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Mtibwa 4-2 mchezo uliochezwa 1992 katika uwanja wa Manungu.