Home news YANGA WAFANYA KWELI BUNGENI…WAIPIGA BAO SIMBA …WAMBEBA JUMLA JUMLA SPIKA TULIA…

YANGA WAFANYA KWELI BUNGENI…WAIPIGA BAO SIMBA …WAMBEBA JUMLA JUMLA SPIKA TULIA…


KLABU ya Yanga leo Februari 18 imefanya uzinduzi wa kadi mpya za Uanachama za kielektroniki kwa Wabunge wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wanachama wa Yanga.

Uzinduzi wa kadi za kielektroniki ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko ya kidigitali na ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kwa mujibu wa katiba ya Yanga toleo Ia 2021.

Hafla ya uzinduzi huo umefanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi ambapo mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ambapo alikabidhiwa kadi mpya ya uanachama.

Itakumbukwa pia, Spika Dk Tulia ni mwanachama na mshabiki kindakindaki wa Simba SC, ambapo mara kadhaa huyaweka mahaba yake kwa Simba SC hadharani.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Wabunge, Viongozi wa Klabu ya Yanga, wadau na waandishi wa habari.

SOMA NA HII  JEMEDARI:- CHAMA AKIZIDIWA UWEZO UWANJANI ANAFANYAGA MAMBO YA KISHAMBA SANA...