MABOSI wa Simba wameweka wazi kuwa kwa sasa mawazo yao yote yapo katika kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali wanayoshiriki ikiwemo ligi kuu ambayo wanapambana na Yanga, hivyo suala la kuwaongezea mikataba mastaa wao wanaomaliza mikataba litapatiwa majibu mwishoni mwa msimu.
Baadhi ya nyota wa Simba ambao wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu ni Bernard Morrison, Taddeo Lwanga, Meddie Kagere, Chis Mugalu, Aishi Manula na Pascal Wawa.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: βNi kweli kuna kundi kubwa la wachezaji wetu ambao wanatarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, hatujaanza mazungumzo nao lakini niwatoe hofu Wanasimba kuwa tunajua nini tunapaswa kufanya juu ya hilo na tutahakikisha wachezaji wote tunaowahitaji kwa msimu ujao wanapewa mikataba mipya.