Home Habari za michezo DAKIKA CHACHE KABLA YA MECHI…PABLO AIBUKA NA HILI SIMBA…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA…

DAKIKA CHACHE KABLA YA MECHI…PABLO AIBUKA NA HILI SIMBA…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA…


WAKATI kocha wa Simba, Pablo Franco akisema wanakwenda kucheza ugenini ili kujihakikisha tiketi ya robo fainali, beki wake wa kulia, Shomary Kapombe amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akisema watawapa raha leo Jumapili.

Simba ipo Benin kwa ajili ya mchezo wao wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast inayocheza mechi zake za nyumbani nchini humo, huku ikiwa kinara wa kundi hilo kwa kukusanya pointi saba.

Kocha Pablo alisema si rahisi kupata ushindi mechi za ugenini katika mashindano hayo kutokana na mambo mengi ya kiufundi ila wamepanga kupata pointi tatu ili kuwa na asilimia kubwa ya kumaliza vinara.

“Tukishindwa kupata pointi tatu basi hata moja kwetu ni muhimu na hilo linawezekana kama ambavyo tulifanya Niger,” alisema Pablo na kuongeza;

“Simba tukimaliza vinara wa kundi tunaweza kuanzia ugenini robo fainali na kumalizia nyumbani hata mpinzani wetu hatakuwa kinara kwenye kundi lake na jambo jingine tutaweka rekodi ya kumaliza vinara.”

Lakini Kapombe alisema tangu walivyomalizana na RS Berkane wamejipanga kuona wanafanya makubwa dhidi ya Asec, licha ya rekodi ya wenyeji wao kuwatisha wanapokuwa nyumbani.

“Mechi za ugenini itakuwa ngumu hilo wachezaji na benchi la ufundi tunalifahamu, tunataka kutimiza malengo yetu ya kwenda hatua inayofuata, mashabiki wasiwe na hofu kwani tutapambana kwa kila hali,” alisema Kapombe.

SOMA NA HII  ISHU YA MAYELE KUUZWA YANGA...INJINIA HERSI AVUNJA UKIMYA..AGUSIA DILI LA KISINDA LILIVYOKUWA..