Home news KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO NA WAMOROCO…PABLO AWAJAZA UPEPO MASTAA SIMBA..AINGIA UBARIDI..

KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO NA WAMOROCO…PABLO AWAJAZA UPEPO MASTAA SIMBA..AINGIA UBARIDI..


Kuelekea mchezo wao wa Jumapili hii dhidi ya RS Berkane ya Morocco kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameshtukia jambo katika mfumo wa uchezaji wa kasi wa Berkane na kuja na plani ya kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa na kasi kubwa ya kushambulia na kulinda.

Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba ambao mpaka sasa wamekusanya pointi 4 katika michezo mitatu waliyocheza, wanatarajiwa kuvaana na RS Berkane siku ya Jumapili katika mchezo huo wa ne wa Kundi D.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara ambao wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao 34 walizokusanya kwenye michezo 16 waliyocheza mpaka sasa, leo Jumatatu wanatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam kuvaana na Dodoma Jiji katika mchezo wao wa 17.

Kocha Pablo alisema: “Tunatarajiwa kuwa na mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Jumatatu (jana), kabla ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.  

“Kwa kuangalia namna ambavyo tulicheza nao kule Morocco, ni wazi kuwa tunatarajia mchezo mgumu lakini ni lazima tuhakikishe tunashinda mchezo huu, tunajua ubora wao katika kucheza mpira wa kasi, hivyo tumekuwa tukiiandaa timu kuhakikisha tunashambulia na kulinda kwa kasi zaidi yao.”

SOMA NA HII  MWAKA MMOJA TOKA ASEPE YANGA....YACOUBA AANIKA SIRI KIBAO YA AZIZ KI...