Home news SOKA LA WANAWAKE: YANGA WAIJIBU SIMBA KIBABE…NYOTA WAKE APATA SHAVU TIMU KUBWA...

SOKA LA WANAWAKE: YANGA WAIJIBU SIMBA KIBABE…NYOTA WAKE APATA SHAVU TIMU KUBWA ULAYA…


NYOTA wa kikosi cha Yanga Princes, Aisha Khamis Masaka amepata dili la kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya BK Hacken FF ya nchini Sweden.

Nyota huyo ni miongoni mwa mastaa ambao walikuwa wakifanya vema kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania na alikuwa anaitwa Asha Magoli kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa hatua hiyo ni kubwa na wamempa hongera Asha kwa kupata timu mpya na kwenda kuanza changamoto mpya.

β€œKlabu ya Yanga inamtakia kila la kheri mshambuliaji wetu Asha Masaka anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa bila majaribio kwenye Ligi Kubwa za Wanawake Barani Ulaya.

β€œNyoya huyo atakuwa ndani ya Klabu ya BK Hacken FF inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Sweden kwa makubaliano maalumu.

β€œBK Hacken FF ni Mabingwa wa Ligi Kuu Wanawake Sweden msimu wa 2020 na wamekuwa wakishiriki UEFA Champions League na mwaka huu wametolewa na Manchester City,” ilieleza taarifa iliyotolewa na Yanga.

Miezi ya hivi karibuni, Simba Queens waliruhusu wachezaji wao wawili kwenda ulaya kufanya majaribio na kujiunga na timu za wanawake za huko.

Kila la kheri Asha kwenye changamoto yako mpya.

SOMA NA HII  AMBOKILE APEWA MWEZI MMOJA NKANA