Home Uncategorized JEMBE LA KAZI YANGA KUTOKA BURKINA FASO LATIA TIMU BONGO RASMI

JEMBE LA KAZI YANGA KUTOKA BURKINA FASO LATIA TIMU BONGO RASMI

 

YACOUBA Sogne mshambuliaji wa Yanga amewasili  Tanzania leo Agosti 31 akitokea nchini Burkina Faso.

Sogne anaungana na wachezaji wenzake kambini jumla kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.

Yanga itaanza na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Septemba 6, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Sogne ambaye amesaini dili la miaka miwili amesema kuwa anafurahi kuwa sehemu ya timu na anafurahi kwa mapokezi.

SOMA NA HII  SIMBA NA CHAMA SASA ISHU IKAE HIVI TU