Home Uncategorized BOSI ZINEDINE ZIDANE ANATIMIZA LEO MIAKA 48

BOSI ZINEDINE ZIDANE ANATIMIZA LEO MIAKA 48


23 Juni,1973, Zinedine Zidane raia wa Ufarasa aliletwa duniani,hivyo leo ni mfanano wa siku yake ya kuzaliwa.

Anatimiza umri wa miaka 48 akiwa ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Real Madrid inayoshiriki La Liga.

Nafasi aliyokuwa anacheza ndani ya uwanja ni kiungo mshambuliaji ambapo kwenye maisha yake ya soka jumla amefunga mabao 95 akiwa amecheza mechi 506.

Msimu wa 1989-1992 alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Cannes ambapo alicheza mechi 61 na kufunga mabao sita, 1992-1996 alikipiga ndani ya Bordèaux alicheza mechi 139 na alitupia mabao 28.

1996-2001 alikipiga Juventus alicheza mechi 151 na alifunga mabao 24 alihitimisha safari yake ndani ya Real Madrid msimu wa 2001-2006 alicheza mechi 155 alitupia mabao 95.

SOMA NA HII  ISHU YA MORISON NGOMA NZITO, MASHABIKI WAJITOKEZA, DIFENDA IPO TFF