Home Uncategorized PRINCE DUBE KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA AJILI YA MATIBABU ZAIDI

PRINCE DUBE KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA AJILI YA MATIBABU ZAIDI


 MHAMBULIAJI namba moja wa Klabu yaAzam FC, Prince Dube, anatarajiwa kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.


Dube mwenye mabao sita na pasi nne za mabao kati ya 18 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili na pointi 25 aliumia kwenye mchezo dhidi ya Yanga jana Novemba 25.


Dube raia wa Zimbabwe, aliumia dakika ya 15 kwa kuvunjika mfupa wa mbele wa mkono wake wa kushoto unaoitwa Ulnar.

Huu ni mfupa unaoanzia kwenye kiwiko na kushuka hadi kwenye kidole cha mwisho.

Taarifa rasmi kutoka Uongozi wa Azam FC imeeleza kuwa Dube ataondoka nchini Jumapili, Novemba 29 kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways (KQ).

Atatibiwa kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo Cape Town, chini ya daktari bingwa wa mifupa, Robert Nicolas.

Azam FC imekuwa ikiitumia hospitali hii kutibia wachezaji wake tangu mwaka 2011.

Uongozi wa Azam FC unampa pole na kumtakia matibabu mema na kupona haraka, Prince Dube.


Pia familia ya michezo Tanzania inamuombea Kheri Dube ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ndani ya Azam FC ambayo ilipoteza mchezo wake jana kwa kufungwa bao 1-0 ikiwa Uwanja wa Azam Complex.
SOMA NA HII  KAGERE ATAJA SABABU YA KUFUNGA MABAO NDANI YA LIGI KUU BARA