Home Habari za michezo ABDI BANDA – SINA MPANGO NA SIJAWAHI KUWAZA KURUDI SIMBA…NI CHUKI TU...

ABDI BANDA – SINA MPANGO NA SIJAWAHI KUWAZA KURUDI SIMBA…NI CHUKI TU DHIDI YANGU….SIWADAI…


Mlinzi wa kati wa Klabu cha Mtibwa Sugar, Abdi Banda amekanusha taarifa zilizochapishwa na jarida maarufu la mtandano la Afrika Kusini la The Kick , ambalo lilimnukuu akiielezea vibaya Klabu ya Simba kuelekea mchezo ujao wa Robo Fainal ya Kombe la Shirikisho Afrika , dhidi ya Orlando Pirates.

Jarida hili maarufu kwa habari za michezo na burudani, lilimnukuu Banda, kuwa Orlando wanapaswa kuwa makini na Simba, kwani mara nyingi hutumia mbinu chafu na wanasiasa kushinda mechi zao kwenye Uwanja wa Mkapa.

Banda amekanusha taarifa hiyo alipozungumza na Mwandishi na mchambuzi wa habari za michezo nchini Abduly Mkeyenge, ambapo amesema kuwa taarifa hiyo ni uzushi, ambao watu wenye lengo baya naye wameamua kuusambaza.

Kupitia ukurasa wake wa kijami wa Facebook, Mkeyenge amemnukuu Abdi Banda kwa maneno hayo hapo chini.

” Kumbe ndiyo maana nilikuwa naona matusi mengi sana sikujua nini chanzo  chake. Mimi sihusiki na chochote cha huko mtandaoni labda kuna mtu ametumia jina langu kwa lengo lake.  

” Sina chuki na wala sijawahi kuwaza kurudi Simba au kuwaomba nirudi, ila kuna wimbi la chuki limesambazwa toka nilivyoondoka Simba. Naonekana kama nina chuki nao yaani hata kikitokea kitu basi inatafsiriwa tofauti.

“Ila kuna chuki imesambazwa kubwa sana kuhusu mimi. Nikipost kitu mtandaoni wanatafsiri wanavyotaka, nikifanya interview basi watachukua maneno machache na kunihukumu nayo. Mimi siidai Simba na wala wao hawanidai na sina chuki nao sababu sijawaza kurudi kwao lakini tusifikie huku. Mimi niongee na Orlando Pirates nawajua wapi ukiacha kucheza ligi ya SA tu? 

” Sababu wanajua mtu waliemzushia ndiyo wanayemtaka kwa hiyo hawakutaka kujiridhisha au kutafuta uhakika basi wakaona wasambaze chuki tu. Ila nashukuru Simba wenyewe hawakuamini mpaka walivyouliza. Hivi sasa baadh yenu (Waandishi) mnafanya wengine waonekane hawana weledi kwa ajili ya  kucopy na kupest vitu bila ushahidi kwa ajili ya kujipatia followers.

” Haina ukweli hiyo taarifa ila wale watu wa smartphone na kupost wanaifanya taaluma yenu idharaulike sababu hawajui uandishi ni nini kaka, ila ni jambo baya, lakini nashukuru maana uongo huwa haukai muda mrefu unakufa” Abdi Banda 

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO KLABU MATAJIRI WA MOROCCO, WALIVYOAMUA KUISAIDIA SIMBA ILI WAIMALIZE BERKANE KESHO...