Home Habari za michezo FT: COASTAL UNION 1- 2 SIMBA SC….’KIFARU CHA KINYARWANDA’ CHAIOKOA SIMBA…WAGOSI WALIBANA…

FT: COASTAL UNION 1- 2 SIMBA SC….’KIFARU CHA KINYARWANDA’ CHAIOKOA SIMBA…WAGOSI WALIBANA…


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wameitandika Timu ya Coastal Union magoli 2-1 katika Uwanja wa Mkwakwani jioni ya leo.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu uliwashahudia Simba wakiwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Bernard Morisson kipindi cha kwanza.

Kipindi cha Pili Coastal walirudi kwa utulivu na kufanikiwa kusawazisha goli dakika ya 78 kupitia kwa Victoa Akpan, akifunga bao maridadi kwa mpira wa kona fupi.

Meddie Kagere A.K.A ‘Kifaru cha kinyarwanda’ akawahakikishia Simba kuondoka na alama tatu baada ya kupachika goli la ushindi dakika ya 93 akiunganisha mpira wa Mugalu.

Ushindi huo unawafanya Simba kufikisha alama 40 baada ya kucheza michezo 18 na wako nafasi ya Pili nyuma ya vinara Yanga wenye alama 51.

Coastal katika mchezo wa leo walimaliza wakiwa pungufu baada ya nahodha wao kuoneshwa kadi nyekundu.

SOMA NA HII  MAJERAHA YA LUKOSA YAMFANYA GOMES 'KUWEWESEKA'