Home news FT: YANGA 0-0 SIMBA….MAYELE AFANYIWA ‘ROHO MBAYA’ NA INONGA…CHAMA ‘ASHINDWA KUPUMUA…’

FT: YANGA 0-0 SIMBA….MAYELE AFANYIWA ‘ROHO MBAYA’ NA INONGA…CHAMA ‘ASHINDWA KUPUMUA…’


Dakika 90 zimekamilika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam huku zikishuhudia mechi ya watani wa Jadi kati ya Yanga na Simba zikienda sare ya bila kufungana.

Licha ya Mabadiliko yaliyofanywa na walimu kipindi cha pili bado hakuna dalili zilizoonesha kama kuna timu iliyokaribia kupata bao.

Idara za ulinzi zilifanya vyema majukumu yao hali iliyofanya kutokuwa na mashuti mengi yaliyolenga lango kwa kila upande.

Kwa kuzingatia ubora wa kazi hiyo, Mshambuliaji kinara wa Yanga, Mayele ameshindwa kufurukuta leo hii ambapo mabeki wa Simba wlaijitahidi kumdhibiti.

Hali kama hiyo pia imekuwa kwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ambaye naye kutokana na shughuli kuwa pevu alishindwa kumaliza mchezo huo, ambapo alifanyiwa ‘sub’ na nafasi yak kuchukuliwa na Rally Bwalya.

Kwa sare hii Yanga wanafikisha alama 54, na Simba anafikisha alama 42 na kufanya pengo la alama kuwa 13 baina yao.

SOMA NA HII  KISA KUPEWA UNAHODHA...MAYELE AANDIKA HISTORIA HII MPYA YANGA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here