Home Azam FC GEORGE MPOLE AZIDI KUMKIMBIZA MAYELE KIMYA KIMYA…AZAM BADO SANA MECHI ZA MIKOANI…

GEORGE MPOLE AZIDI KUMKIMBIZA MAYELE KIMYA KIMYA…AZAM BADO SANA MECHI ZA MIKOANI…


Geita Gold FC na Azam FC zimegawana alama moja moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara uliochezwa jana Jioni katika dimba la Nyankumbu mkoani Geita baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Wenyeji wa mchezo huo Geita ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 26 kupitia kwa George Mpole ambalo ni bao lake la 11 kwenye Ligi Kuu, Azam FC wakasawazisha bao hili dakika ya 35 kupitia kwa Ismail Kader, timu hizo zikaenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili zikiwa zimesalia dakika 8 mchezo kumalizika kunako dakika ya 82 Danny Lyanga akaifungia Geita bao la pili lakini dakika 7 baadae dakika ya 89 Chilo Mkama wa Geita akajifunga na kuipatia Azam bao la pili la kusawazisha na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 2-2.

Kwa matokea haya Azam imefikisha alama 29 katika michezo 20 wamepanda kutoka nafasi ya 5 hadi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na alama sawa na Namungo walionafasi ya 3. Geita wamefikisha alama 28 na wamesalia nafasi ya 6.

SOMA NA HII  MAYELE AENDELEA ALIPOISHIA ...ATIA KAMBANI GOLI TATU MWENYEWE....AZIZ KI , MAKAMBO WANOGESHA 'SHOW'....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here