Home Habari za michezo KISA KUTOLIONA GOLI TOKA MSIMU HUU UANZE…MORRISON ‘AMCHONGEA’ BOCCO SIMBA…

KISA KUTOLIONA GOLI TOKA MSIMU HUU UANZE…MORRISON ‘AMCHONGEA’ BOCCO SIMBA…


Winga fundi wa Simba, Bernard Morrison ‘BM3’ ametumia siku 322 kufunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Bara baada ya juzi kuifanyizia Coastal Union, huku akimchongea nahodha wake, John Bocco ambaye hajafunga bao tangu Julai 18, 2021.

Morrison aliifungia Simba bao la kwanza kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga kabla ya Meddie Kagere itupie la pili na la ushindi wakati wakiizima Coastal kwa mabao 2-1.

Mara ya mwisho kwa Morrison kufunga bao ilikuwa msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Mei 21, 2021 na kuhaha karibu miezi 10 na ushei bila ya bao kabla ya juzi kufunga.

Mbali na kutumia muda mrefu kuifungia timu yake kwenye michezo ya ligi Morrison ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi kwenye mashindano ya kimataifa wanayoshiriki akifunga mabao 3 na kutoa pasi za mwisho nne.

Pia winga huyo kwenye michezo 18 waliyocheza ni mechi sita tu ameanza kikosi cha kwanza ambazo ni dhidi ya Namungo, Ruvu Shooting, Yanga, Mbeya City, Kagera Sugara na Coastal Union.

Bao la Morrison ni kama limemchongea Bocco ambaye hana bao katika Ligi licha ya msimu uliopita kuibuka Mfungaji Bora akifunga mabao 16. Bocco ana mabao mawili aliyofungwa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneg Galaxy.

SOMA NA HII  FT:SIMBA 3-0 COASTAL UNION....'KOMBINESHENI' YA CHAMA NA MIQUISSONE MHH...!!