Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA MECHI NA AZAM KUANZA…YANGA KUKOSA MAJEMBE YAKE YOTE...

SAA CHACHE KABLA YA MECHI NA AZAM KUANZA…YANGA KUKOSA MAJEMBE YAKE YOTE MUHIMU..HAWA HAPA…


Vinara wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Yanga SC itawakosa wachezaji takribani wa nne kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC unaochezwa leo Aprili 06, 2022. Uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Da es salaam.

Kukosekana kwa Aucho, Bangala na Feisal, Yanga imesalia na vingo wa kati wawili tu ambao wapo fiti kucheza leo ambao ni Zawadi Mauya na Salum Abubakari Sure Boy.

Kocha msaidi wa Yanga Cedric Kaze amethibitisha kuwa kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC watawakosa wachezaji Feisal Salum ‘Fei Toto, Khalid Aucho kutokana na majeruhi lakini pia mchezaji Yannick Bangala Litombo aliumia juzi mazoezini watamuangalia kama ataweza kucheza leo na Faridi Musa anaumwa.

Kocha kaze pia amesema wachezaji Crispin Ngushi, Abdallah Shaibu ‘Ninja, jesus Moloko wate wanafanya mazoezi na timu pamoja na wachezaji wengine wote baada ya kupona majeruhi na wataangalia kama watakuwa vizuri kuwa sehemu ya mchezo wa huu.

Kukosekana kwa Aucho, Bangala na Feisal kuna ifanya Yanga kusalia na vingo wa kati wawili tu ambao wapo fiti kucheza leo ambao ni Zawadi Mauya na Salum Abubakari Sure Boy.

Yanga ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 48 na wanaongoza kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Simba SC walio nafasi ya pili, huku timu ya wanachi wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wamewazidi Azam FC alama 20, na mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga ilishinda mabao 2-0 mchezo uliochezwa uwanja wa benjamini mkapa.

SOMA NA HII  YANGA BADO TATU TU....