Home Habari za michezo BAADA YA MECHI NA AZAM KUISHA KWA SARE…PABLO APATA CHA KUSINGIZIA SIMBA….AWATAJA...

BAADA YA MECHI NA AZAM KUISHA KWA SARE…PABLO APATA CHA KUSINGIZIA SIMBA….AWATAJA KINA KAGERE…


PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa tatizo ambalo linamsumbua kwa sasa ni ubora wa wachezaji wake hasa kwenye safu ya ushambuliaji.

Kwenye mchezo wao mzunguko wa pili dhidi ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex uliochezwa Mei 18, mabingwa hao watetezi walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Ni Rodgers Kola alifunga dk ya 37 kwa upande wa Azam FC kisha lile la Simba lilifungwa na John Bocco na kufanya kwenye msako wa pointi tatu wagawane pointi mojamoja.

Pablo amesema:”Tumekuwa kwenye mwendo ambao hatujaupenda na tulipata nafasi mbele ya Azam FC lakini tumekwama kuzitumia hili ni tatizo.

“Ubora wa safu ya ushambuliaji kutoweza kutumia nafasi ambazo tumezitengeneza ni sababu ya kushindwa kupata matokeo, kwa hili tutalifanyia kazi kwa mechi zijazo,”

 Simba inafikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo huku Azam FC ikiwa na pointi 33 nafasi ya 5 kwenye msimamo.

SOMA NA HII  MABASI KUTOKA AFRIKA KUTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA QATAR...FAINAL ZIKISHA YATAGAWIWA BUREEE...