Home Habari za michezo ISHU YA KUTOROKA KAMBINI…AMBUNDO AANIKA KILA KITU WAZI…ADAI MLINZI ‘KAWACHOMESHA’….

ISHU YA KUTOROKA KAMBINI…AMBUNDO AANIKA KILA KITU WAZI…ADAI MLINZI ‘KAWACHOMESHA’….


Dickson Ambundo ambaye ni mmoja ya wachezaji wa Yanga wanaotajwa kufukuzwa katika kambi ya timu hiyo amesema kuwa yeye alimuomba ruhusa ya kutoka kwa mlinzi ila mlinzi ndo amefikisha taarifa za uongo kwa viongozi

Ambundo amesema; “Niliomba ruhusa kwa mlinzi, niliagiza gari yangu na ikaja mpaka kambini sikumuona kiongozi hivyo nikamuomba mlinzi ruhusa nikatoka kuchukua gari na kila mtu aliona wakati naendesha, sema mlinzi ndo kazingua kafikisha taarifa sio za kweli,” amesema Ambundo.

Ambundo na mwenzake Saido Ntibazonkiza walisimamishwa juzi na Kocha Mkuu wa Yanga, kwa kile alichodai kuwa wachezai hao walitoroka kwa siri na kwenda kusiko julikana.

Katika Jitihada za kutaka kuyamaliza mambo, wachezaji kadhaa wa Yanga wakiongozwa na Fiston Mayele walimuendea Kocha Nabi na kumtaka awasemehe wachezaji hao, lakini Nabi aliwakatalia huku akiweka wazi msimamo wake wa kutowatumia wachezaji hao kwenye mechi ya kesho dhidi ya Simba.

Jambo hili linaweza kuigharimu Yanga kwenye kikosi cha kesho, kwani inaeleweka fika umuhimu wa Saido Ntibazonkiza kwenye kikosi cha Kwanza cha Yanga , ambapo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kutengeneza mashambulizi.

Hali kadhalika kwa Ambundo, ambaye naye amekuwa na msaada mkubwa sana Kwenye kikosi hicho cha mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu,kwani kwa siku za hivi karibuni amekuwa akifunga magoli muhimu ya kuisaidia timu kupata ushindi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO....AUSSEMS AIUA SIMBA MAPEMAA...AIBETIA YANGA USHINDI WA KISHINDO...