Home Uncategorized NALDO MAMBO YAMEGOMA KWENDA HUKO AZAM FC

NALDO MAMBO YAMEGOMA KWENDA HUKO AZAM FC


IDD Seleman, ‘Naldo’ nyota anayekipiga ndani ya Azam FC kwa sasa mambo kwake yamekuwa magumu kwa kushindwa kucheka na nyavu kama zamani.

Msimu uliopita wa 2018/19 alipokuwa ndani ya Mbeya City alikuwa ni mbadala wa Eliud Ambokile ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya TP Mazembe ya Congo na alisepa akiwa ametupia mabao 10.

Naldo msimu huo alitupia mabao 10 jambo lililowavuta mabosi wa Azam FC na akamwaga wino hapo alipo kwa sasa.

Mambo yamekuwa magumu kwani kwa sasa ametupia mabao matano kimiani na mabosi hao wa Azam FC wamebakiwa na mechi 10 pekee kukamilisha mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  PSG: ISHU YA NEYMAR KUTAKA KUSEPA ILIKUWA INAJULIKANA KITAMBO