Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI ULAYA…WAKALA ASHINIKIZA LEWANDOWSKI KUTUA BARCELONA…ANUNUA JEZI KUMI ZA BARCA….

TETESI ZA USAJILI ULAYA…WAKALA ASHINIKIZA LEWANDOWSKI KUTUA BARCELONA…ANUNUA JEZI KUMI ZA BARCA….


Wakala wa Robert Lewandowski, Pini Zahavi ameripotiwa kununua jezi 10 za klabu ya Barcelona zilizochapishwa jina la mshambuliaji huyo kwenye duka rasmi la klabu ya Barcelona kwa mujibu wa Gerrard Moreno.

Wakala huyo amekuwa akiishinikiza Bayern Munich kumwachia nyota huyo huku akiripotiwa kufanya mazungumzo na Barca juu ya mustakabali wa Lewandowski.

Hatua hii inazidi kuchochea uvumi wa Lewandowski kwenda Barcelona. Mkataba wa Lewandowski unamalizika msimu ujao huku ikielezwa kuwa anataka kuondoka klabuni hapo.

SOMA NA HII  SAKATA LA MORRISON YANGA....NABI AKOLEZA CHUMVI....KAMKATAA MCHANA KWEUPEEE....