Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba amesema kuwa ataenda kuonyesha kiwango kizuri kwenye klabu atakayojiunga nayo ili Manchester United waone walifanya kosa kutomuongezea mkataba mpya wa kubakia klabuni hapo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi huu ambapo pamoja na kuwekewa mkataba mnono wenye thamani ya pauni laki tatu (300,000) kwa wiki bado hakuwa tayari kuongeza kandarasi mpya klabuni hapo.
Akizungumza katika moja ya vipande ambavyo vimeandaliwa kwenye makala yake Pogba amesema anataka kuonyesha kiwango bora ili nionyeshe namna nilivyokuwa muhimu hata Manchester.
“Nitafanya vizuri katika klabu ambayo nitaenda kujiunga nayo ili niionyeshe dunia kuwa bado nina uwezo wa kucheza na kuleta matokeo kwa timu tofauti na ninavyofikiriwa”.
Pogba alijiunga kwa mara ya kwanza mwaka 2009 akitokea Le Havre akiwa na miaka 16 kabla ya kuondoka klabuni hapo kwenda Juve 2012 kama mchezaji huru lakini alikuja kusajiliwa tena mwaka 2016 kwa kitita cha pauni milioni 89.
Hata hivyo pamoja na kusajiliwa kwa hela ndefu bado kwa kipindi chote hicho Pogba alishindwa kuonyesha kiwango kizuri kwa mfululizo zaidi ni kuibuka na kushuka.