Home Habari za michezo KOCHA WA MAMELOD SUNDOWN AITIA SIMBA AIBU SAUZI…YAONEKANA NI TIMU ‘INAYOJITUTUMUA’ LAKINI...

KOCHA WA MAMELOD SUNDOWN AITIA SIMBA AIBU SAUZI…YAONEKANA NI TIMU ‘INAYOJITUTUMUA’ LAKINI HAINA PESA…


Inafahamika kuwa Simba ina majina mawili makubwa ya makocha mezani, mmojawao atatangazwa kabla ya wikiendi ijayo.

Lakini Wekundu hao wamekuwa gumzo kubwa kwa sasa kwenye vyombo vya habari vya Afrika Kusini mjadala ukiwa ni jinsi inavyoshindwa kutanua misuli ya kifedha kupambana na matajiri wa nchi hiyo.

Klabu nyingi za nchi hiyo zimewekeza fedha nyingi kutoka kwenye vyanzo binafsi pamoja na wadhamini jambo ambalo limepandisha thamani za wachezaji mpaka makocha kuwa tofauti na ligi nyingine za Afrika. Simba inasuka upya benchi la ufundi tayari kwa usajili mpya wa wachezaji baada ya kutemana na Pablo Franco ambaye ni Mhispania.

Licha ya kwamba wamekuwa wakiendesha zoezi hilo kwa usiri mkubwa lakini limekuwa mjadala miongoni mwa wachambuzi na vyombo vya habari nchini humo hasa inavyojaribu kutunisha msuli kujitofautisha na klabu zingine za Afrika Mashariki. Taarifa za magazeti, mitandaoni na hata baadhi ya televisheni zinadai Simba inapambana kupata kocha bora wa thamani ya kawaida inayoendana na uwezo wake wa kiuchumi ndio maana wengi wamekwama kumalizana nao pamoja na wengine kwa wakati.

Habari za uhakika ni kwamba Simba inamtaka Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena ambaye ni Msauzi, lakini kikwazo ni dau kubwa la mshahara huku akiwa na mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ingawa amewaambia yuko tayari kuondoka muda wowote.

Simba ilitua kwa Mokwena baada ya kutemana na Stuart Baxter aliyewahi kuifundisha Kaizer Chiefs ambaye pia dau lake ni pasua kichwa kwa uchumi wa klabu ya Ligi Kuu Bara.

Habari zinasema mawakala na mameneja wa makocha wamekuwa wakivujisha habari kwenye vyombo vya habari kwamba dau la mishahara ya Simba waliyowaambia wateja wao ni midogo tofauti na umaarufu na mafanikio yake Afrika ingawa baadhi ya wachambuzi wamedai Simba kupitia changamoto hizo ndiyo inaanza kukua.

Mmoja wao alidai Simba inataka kumlipa Mokwena chini ya Sh10 milioni kwa mwezi ambayo ni ndogo kwani analipwa zaidi ya Sh70 milioni kila mwezi mbali na marupurupu.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA NYONI KUTEMWA SIMBA....MBRAZILI KAMTAZAMA WEE...KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HILI..

Habari zinasema Simba bado ina mawasiliano ya karibu na Mokwane ili awatafutie kocha mwingine ambaye inadawa ni nje ya Sauzi.

Picha ya CEO wa Simba akiwa na mmoja wa makocha hao imesambaa ingawa ishu ya Sven Vandebroek kuwashtaki Simba Fifa mwaka jana akidai Dola 44,000 (zaidi ya Sh100 milioni) nayo imeonekana kuibua mjadala kwa madai kwamba kwa klabu za Sauzi ni fedha ndogo.