Home Habari za michezo PAMOJA NA RAIS WA YANGA INJINIA HERSI KUKATAA MAYELE KUSEPA…WAARABU BADO WAVIZIA...

PAMOJA NA RAIS WA YANGA INJINIA HERSI KUKATAA MAYELE KUSEPA…WAARABU BADO WAVIZIA NAMNA YA KUSEPA NAYE…


Straika wa Yanga, Fiston Mayele juzi mchana aliondoka nchini kwenda kwao DR Congo, kwa mapumziko mafupi, huku akisikilizia ofa yake ya kwenda Sudan baada ya matajiri wa Kiarabu kuweka mzigo wa maana wakimtaka ili akaitumikie Al Hilal kwa msimu ujao.

Mayele aliyemaliza kama mfungaji bora wa Yanga na kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu akiwa nyuma ya George Mpole wa Geita Gold, awali alikuwa akitakiwa na matajiri wa RS Berkane ya Morocco, lakini mabosi wa klabu hiyo wa Jangwani wakaipotezea ofa hiyo.

Straika huyo ambaye bao lake limetwaa tuzo za Ligi Kuu 2021-2022, alitua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na amebakisha mwaka mmoja ambao Al Hilal wanataka kuununua.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, Wasudan wapo tayari kutoa Dola 200,000 (zaidi ya Sh 600 milioni) kuununua mkataba huo, kisha kumpa Mayele mkataba wa miaka minne ambao utakuwa wa thamani ya dola 90,000 kila mwaka mbali na mshahara wa dola 5,000 kwa mwezi sambamba na usafiri, malazi na bonasi nyingine nono.

Mtu wa karibu wa mchezaji huyo alidokeza kuwa, mmoja wa viongozi wa Al Hilal alishawasiliana na vigogo wa Yanga na hata kumdokeza mchezaji mwenyewe, lakini vigogo hao wa Jangwani msisitizo wao ni kwamba hawamuuzi Mayele kwa vile wana mashindano.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa alisema hivi karibuni kwamba hawana mpango wa kumuachia mchezaji huyo kwani wana mipango nae kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.

SOMA NA HII  'KWA YANGA HII YA MAYELE, 'FEI TOTO' MOLOKO, AUCHO...HATA WAJE LIVERPOOL HAWATOKI KWA MKAPA'...