Home Habari za michezo ULISIKIA ISHU YA MOSIMANE NA YANGA..? BASI UKWELI WA MCHONGO WOTE NA...

ULISIKIA ISHU YA MOSIMANE NA YANGA..? BASI UKWELI WA MCHONGO WOTE NA KAZI ANAYOKUJA KUIFANYA UKO HIVI…


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini ameitikia ombi la Klabu ya Yanga na kuthibitisha kuwa atahudhuria katika wiki ya Mwananchi itakayofanyika Agosti 6, 2022 jijini Dar es Salam.

Ikumbukwe kuwa, Juni 26, 2022, Pitso aliipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC na kufanya gwaride la heshima huku akisema kuwa Afrika nayo inaweza kufanya magwaride yao ya Ubingwa kama Ulaya.

Pitso aliongeza kuwa angetamani kuja Tanzania kutazama mechi ya Yanga SC na Coastal Union fainali ya FA lakini majukumu yamembana akaomba link ya kutazama mechi hiyo. Hata hivyo aliomba kujua Ratiba ya Simba na Yanga ili kuja Tanzania kuutazama mchezo huo.

SOMA NA HII  FUNGUA VYUMBA 25 VYA HOT SHOT UWE MILIONEA WA LEO KUPITIA MERIDIANBET CASINO...