Home Habari za michezo VITA VYA UKRAINE VYAMFANYA STRAIKA KUTAFUTA TIMU YA KUCHEZA BONGO…FIFA WAMPA BARAKA...

VITA VYA UKRAINE VYAMFANYA STRAIKA KUTAFUTA TIMU YA KUCHEZA BONGO…FIFA WAMPA BARAKA ZOTE…

 


Straika Yohana Mkomola anayekipiga katika klabu ya Vorskla Poltava ya nchini Ukraine anatajwa yupo mbioni kujiunga na timu za Ligi Kuu kwa mkopo.

Mkomola yupo nchini baada ya vita zinazoendelea nchini Ukraine na sasa anadaiwa tayari ameanza mazungumzo na baadhi ya timu ili kukamilisha dili la kucheza kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mmoja wa marafiki wa karibu na mchezaji huyo alidokeza kuwa Mkomola kwa sasa anafikiria kucheza kwa mkopo nyumbani kisha ndio ajue mambo mengine.

“Kiukweli hajafikilia kwanza kurudi kule kwa sababu ya mazingira namna yalivyo ambayo yalimfanya arudi nyumbani, anataka acheze kwa mkopo hapa kisha aangalie mazingira mengine.”

Ikumbukwe, FIFA wamewapa ruksa wachezaji wote wa Ukraine kujiunga na timu wanayoitaka ili kulinda vipaji vyao wakati wakisubili masuala ya usalama yakae sawa.

Mkomola mwenye umri wa miaka 22 alicheza Kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Gabon.

SOMA NA HII  SIMBA YAPANIA KUFANYA MAKUBWA SEPTEMBA 19 KWA MKAPA