Home Habari za michezo PAMOJA NA KUCHEZA MECHI MBILI TU….ZAHERA KAITAZAMA YANGA WEEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA...

PAMOJA NA KUCHEZA MECHI MBILI TU….ZAHERA KAITAZAMA YANGA WEEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA…


Kikosi cha Yanga kimerejea Dar es Salaam baada ya juzi Jumamosi kumaliza mechi ya pili ya Ligi Kuu kikiandika rekodi mpya ya kucheza michezo 39 bila kupoteza, lakini kocha wa zamani wa timu hiyo amekiangalia kikosi hicho akakilinganisha na Simba kisha akatamka kwa ujasiri jamaa wana timu bora.

Kocha aliyetoa kauli hiyo, Mwinyi Zahera amesema katika mechi mbili za awali tu kwake zimetosha kupata majibu kwamba Yanga bado wataendelea kusumbua kutokana na kikosi walichonacho kulinganisha na wapinzani wao ndani ya Ligi Kuu Bara.

Zahera ambaye ni Mkurugenzi wa soka la vijana wa Yanga alifafanua kauli yake akisema hatua ya Yanga kushinda mechi ya kwanza ya ligi huku ikiwaweka benchi mastaa watano ni jibu kwamba timu yao ina kikosi kilichoshiba.

Yanga ikicheza dhidi ya Polisi ilishinda mabao 2-1 huku wachezaji viungo Feisal Salum, kiraka Yannick Bangala, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Bernard Morrison na Heritier Makambo wakiwa benchi.

“Hao wachezaji ambao walianzia benchi wakienda katika klabu yoyote hapo wanaanza moja kwa moja, angalia Feisal, Bangala, Sure Boy hawa ni wachezaji ambao wanaweza kuanza kikosi cha kwanza na timu ikapata matokeo,” alisema Zahera na kuongeza;

“Hii ina maana Yanga bado ina timu bora na itaendelea kusumbua katika ligi, lakini kikubwa zaidi ina makocha walewale bora ambao waliwapa mafanikio, unaangalia mchezo wao bado ni uleule angalia jinsi wanavyotulia na kutafuta mabao kwa mbinu bora.

Zahera ni kocha wa Timu ya Taifa ya DR Congo aliongeza katika kuwaweka benchi mastaa hao kutawapa presha wale ambao wataanza wakijua kama watafanya makosa kuna watu watachukuia nafasi zao.

“Wale ambao wanaanza sasa hakuna ambaye atafanya kazi ya kawaida kila mmoja atajituma ili aweze kufanya kitu, unaona Mayele alipoteza penalti lakini anarudisha akili anafunga bao zuri, hapa kocha na uongozi wa Yanga umefanikiwa kuweka timu bora ambayo itawapa wachezaji presha ya kupoteza nafasi ya kuanza.

“Wakati una timu bora kama hiyo unaongheza tena watu bora kama kina Azizi KI (Stephane) ambao wanaleta ubora zaidi kwenye timu hii, nafikiri ni suala la muda tu kocha akiwapa ubora zaidi wachezaji watakuwa bora zaidi ya sasa.

SOMA NA HII  FT: YANGA 0-0 SIMBA....MAYELE AFANYIWA 'ROHO MBAYA' NA INONGA...CHAMA 'ASHINDWA KUPUMUA...'

“Simba na Azam wana wachezaji wazuri lakini, angalia kama Simba bado kuna maeneo hawakufanya usajili lakini wana wachezaji wengi wapya na kocha mpya, wachezaji watahitaji muda kujua kipi kocha wao anataka wafanye.”