Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA LIGI KWA NGUVU…STRAIKA WA UKRAINE KAFUGUKA HAYA KUHUSU MAYELE...

BAADA YA KUANZA LIGI KWA NGUVU…STRAIKA WA UKRAINE KAFUGUKA HAYA KUHUSU MAYELE NA JINSI ANAVYOTETEMA


Straika wa Vorskla Poltava ya Ukraine, Yohana Mkomola amesema anaifuatilia Ligi Kuu Bara na kuanika siri za nyota wa Yanga, Fiston Mayele kuwasumbua mabeki wa timu pinzani.

Mkomola aliyerejea nchini kutokana na vita inayoendelea Ukraine dhidi ya Russia, alisema mabeki wengi wanashindwa kumsoma Mayele maeneo anayosimama wakati akitaka kufunga na badala yake wanakomaliza kuufuatilia mpira unakoenda.

“Mayele anajua kukaa kwenye njia ya kufunga, mabeki wengi wanajisahau ndio maana anawazdin ujanja kwani ana mikimbio flani ambayo yamekuwa yakimrahisishia kufunga mabao tangu msimu uliopita,” alisema Mkomola aliyewahi kuichezea timu hiyo akisajiliwa kutoka Serengeti Boys.

Alisema Mayele anatumia akili kama alivyo kiungo wa Simba, Clatous Chama akiwa na mpira mguuni kiasi ni ngumu kujua anataka kufanya nini, ndio maana wanaomkaba wanapisha naye.

Mbali na Mayele, pia Mkomola alimtaja George Mpole wa Geita Gold akisema alijitahidi, hivyo msimu huu anapaswa kuongeza bidii zaidi ili kulinda heshima yake.

“Mpole ni mpambanaji, anajua kufunga anachotakiwa kukifanya kwa msimu huu ni kuwadhihirishia Watanzania kwamba hakubahatisha, kwani kazi yake ni kufunga na kwa namna ligi ilivyo ngumu akifunga zaidi ya mabao aliyofunga msimu uliopita thamani yake itapanda zaidi,” alisema Mkomola aliyekuwa kwenye kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afcon U-17 mwaka 2017.

SOMA NA HII  LIGI YA WANAWAKE IMEKAMILIKA, ZAWADI ZAO WAPEWE KWA WAKATI