Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, baada ya kuachana na aliyekuwa kocha Mkuu Zoran Maki, mchakato wa kumpata mrithi wake umeanza haraka na wanatarajia kuwa naye kabla ya mechi yao ya Kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullet ya Malawi.
Ahmed amesema, kwenye orodha ya makocha ambao waliomba wakati wanatafuta kocha kabla ya msimu huu kuanza, walikuwepo makocha wengine wawili ambao walistahili hivyo wapo kwenye kuangalia yupi yupo sokoni ili waweze kumalizana naye.
βTuna mechi dhidi ya KMC kesho lakini baada ya hapo tutakuwa na mechi ya Klabu Bingwa dhidi ya Nyasa Septemba 10 hivyo tunaimani mpaka tunakwenda kwenye mchezo huo, tutakuwa tumeshakamilisha sehemu kubwa ya benchi ya ufundi,β alisema Ahmed.
Simba wamtangaza kuachana na kocha huyo mapema leo Septemba 6, 2022 sambamba na kocha wa viungo Sbai Karim pamoja na aliyekuwa kocha wa makipa Mohamed Rachid.