Home Habari za michezo BAADA YA TAIFA STARS KUFUNGWA JANA…FEI TOTO AONYESHA RANGI YAKE HALISI…AIBUKA NA...

BAADA YA TAIFA STARS KUFUNGWA JANA…FEI TOTO AONYESHA RANGI YAKE HALISI…AIBUKA NA KAULI HII KWA WATZ…


Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewaomba radhi Watanzania na mashabiki wote wa mpira kufuatia kichapo cha Stars kutoka kwa Timu ya Taifa ya Uganda.

Katika mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la CHAN, ulipigwa nchini Uganda, Stars ilipigwa bao 3-0 na kuondoshwa rasmi katika michuano hiyo.

Mchezo wa kwanza uliopigwa weekendbiliyopita, Stars ilifungwa bao 1-0 na Uganda, hivyo Tanzania imeondoshwa kwa kufungwa na Uganda jumla ya bao 4-0 katika michezo miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Fei Toto ameandika; “Watanzania wenzangu, najua inaumiza, najua inakera, najua maumivu mnayoyapitia sababu mnapenda kuiona timu yetu ya taifa ikifanya vizuri.

“Tulipewa jukumu la kuibeba bendera ya taifa letu tumewaangusha. Nichukue fursa hii kuwaomba radhi, naamini tutafanya vizuri hapo mbeleni,” amesema Fei Toto.

SOMA NA HII  HII SIMBA INABALAA ZITO LIGI KUU MSIMU HUU