WAKATI Simba wakishangilia beki wao Henock Inonga kuwa staa pekee kuitwa kikosi cha DR Congo Burkina Faso wamemkutanisha rasta huyo na kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki.
Azizi KI amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 cha Burkina Faso wataocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo kwenye Uwanja wa Moulay Abdallah jijini Rabat nchini Morocco, Septemba 23.
Kikosi hicho kina wachezaji wanne pekee wanaocheza soka la Afrika ambao ni kutoka nchi za Morocco,Tanzania na Misri.
Katika kikosi hicho wamo makipa watatu ambao ni Koffi Herve( Charleroi-Ubelgiji), Nikiema Kilian ( Ado Den Haag-Uholanzi) na Konate Hillel(Valenciennes-Ufaransa).
Wamo mabeki nane Edmond Tapsoba (Leverkusen-Ujerumani), Dayo Issoufou (RS Berkane,Morocco), Yago Steeve (Aris Limassol-Cyprus), Issa Kabore (Olympic de Marseille-Ufaransa), Abdoul Guiebre (AC Reggiana-Italy), Dylan Ouedraogo (OH Louvain-Ubelgiji), Adama Fofana (Dijon FCO-Ufaransa) na Nagalo Adamo (FC Nordsjaelland-Denmark).
Viungo wako saba Bangre Mamady, Gustavo Sangare ( wote Quevily Rouen, Ufaransa), Toure Blati (Pyramids-Misri), Ouedraogo Ismahilia (Volos NPS-Ugiriki), Salou Dramane (FC Noah Yerevan-Armenia), Bandaogo Abdoul (Club Deportivo Trofense-Ureno) na Aziz KI (Yanga SC).
Pia kuna washambuliaji Saba Badolo Cedric, About Ouattara ( wote FC Sheriff Tiraspol-Moldovan), Betrand Traore (Istanbul Basaksehir-Uturuki), Dango Ouattara (FC Lorient- Ufaransa), Cyrille Bayala ( AC Ajaccio-Ufaransa), Tapsoba Fessal ( Standard Liege-Ubelgiji) na Djibril Ouattara ( RS Berkane, Morocco).