Home Habari za michezo KMC NAO WALAMBA ASALI YA UDHAMINI WA MERIDIAN BET….WASAINI MKATABA MNONO HUJAWAHI...

KMC NAO WALAMBA ASALI YA UDHAMINI WA MERIDIAN BET….WASAINI MKATABA MNONO HUJAWAHI KUTOKEA ….


Klabu ya soka Kinondoni Municipal Football Club ‘KMC’ leo wamesaini mkataba wa udhamini na kampuni ya michezo ya kubahatisha Meridianbet kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo kiasi cha pesa cha udhamini huo hakikuwekwa wazi kwenye press hiyo.

Klabu ya KMC inashiriki ligi kuu ya Tanzania ‘NBC Premier League’ leo kwenye ukumbi wa mikutano wa ndani wa manispaa ya kinondoni uongozi wa KMC umeishukuru kampuni ya Meridianbet kwa udhamini wao kwenye klabu hiyo.

Mkutano wa masainishano ya Mkataba huo, ulihudhuriwa na naibu mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni, kaimu mkurugenzi wa manispaa na mkurugenzi wa meridianbet ambapo kuanzia leo, klabu ya KMC mdhamini wake mkuu itakuwa ni kampuni ya meridianbet hadi mwaka 2025.

Awali kampuni ya Meridianbet ilikuwa inasaidia ligi za mtaani ili kuweza kuibua vipaji ambapo walianzisha mashindano mbalilmbali ikiwemo wamshindano ya vijana na wanawake na pia walishawai dhamini timu ya daraja la kwanza ya Pan African.

SOMA NA HII  YANGA VS RIVERS UNITED KUKIWASHA LEO...HUJUMA ZAWASHTUA WANANCHI