Home Geita Gold FC PAMOJA NA KUJIUNGA NA GEITA GOLD…JINA LA SAIDO NTIBAZONKIZA LATAJWA TENA YANGA…KAZE...

PAMOJA NA KUJIUNGA NA GEITA GOLD…JINA LA SAIDO NTIBAZONKIZA LATAJWA TENA YANGA…KAZE ASHINDWA KUJIZUIA…


KOCHA msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema ujio wa kiungo mshambuliaji, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ kwenye kikosi cha Geita Gold ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo iliyopo Ligi Kuu Bara.

Kaze alisema ubora na uzoefu alionao nyota huyo utakuwa msaada mkubwa kwao huku akiweka wazi urejeo wake nchini ni kuonyesha ni kwa jinsi gani soka la Tanzania linapiga hatua nje ya nchi.

“Ni ngumu kuona mchezaji kama yeye anarudi na kucheza timu kama Geita lakini hii yote inaonyesha timu zina fedha za kuweza kukidhi mahitaji ya mastaa wakubwa,” alisema Kaze na kuongeza;

“Uwepo wake utaongeza chachu na kiu kwa vijana wengi ambao wanahitaji kujifunza kutoka kwake na kufikia mafanikio ambayo amefikia.”

Mwenyekiti wa Geita Gold, Leonard Bugomola alisema licha ya usajili wa staa huyo kuchelewa kuingizwa kwa ajili ya michezo ya kimataifa ila bado hawana shaka juu ya hilo kwani ataendelea kuonyesha ushindani katika michuano ya ndani.

Kabla ya kutua Geita Gold, Saido alikuwa akiichezea Yanga ambapo aliachana nayo Mei Mwaka huu kutokana na mkataba wake kumalizika huku akicheza michezo 18 kati ya 30 ya Ligi Kuu Bara na kufunga mabao saba na kuchangia matatu (assisti).

SOMA NA HII  CHE MALONE AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU BIFU LAKE NA INONGA